March 29, 2016


Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja amesisitiza mchezaji lazima awe na nidhamu na hilo halina mjadala kwake.

Akasisitiza kuwa Hassan Isihaka amerejea katika kikosi chake na anafanya kazi vizuri sana kwa kuwa ameelewa yeye anataka nini.

“Tunaendelea vizuri sana na Isihaka, anafanya mazoezi na wenzake na mambo yanakwenda vizuri. Hiki ndicho ninachotaka kwa kuwa kwangu nidhamu ni namba moja kwangu.

“Isihaka tunaye na hana tatizo, anaendelea vizuri. Bado naendelea kusisitiza suala la nidhamu ni muhimu kabisa katika kazi yangu,” alisema Mayanja.Isihaka amerejea kundini Simba baada ya kuwa amesimamishwa baada ya kumjibu maneno yasiyo ya kiungwana kocha huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV