Pamoja na ugumu wa mechi dhidi ya Prisons katika Kombe la Shirikisho, Uongozi wa Azam FC, umesema unataka ushindi na umewaita mashabiki wake.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema wanataka kushinda mechi hiyo na wamejiandaa hasa.
"Mashabiki wetu waje kwa wingi kutuunga mkono. Tumejiandaa kwa ajili ya mechi hiyo ingawa tunajua ubora wa Prisons lakini sisi tuna kikosi bora zaidi," alisema.
Mechi hiyo ya Azam FC na Prisons inasubiriwa kwa hamu kwa kuwa inakutanisha timu zenye kiwango cha juu katika ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment