March 31, 2016



Yanga inashuka uwanjani leo kupambana na Ndanda FC katika mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD bila ya wachezaji wake wawili muhimu wa kigeni.

Yanga itawakosa mshambuliaji wake Mrundi, Amissi Tambwe na kiungo Myarwanda Haruna Niyonzima.

Kocha Msaidizi wa Yanga: "Niyonzima na Tambwe walikuwa na majukumu ya kitaifa, walikwenda kuzitumikia timu zao za taifa.

"Wamechelewa, hivyo hatutakuwa nao katika mechi dhidi ya Ndanda. Hata hivyo tumefanya maandalizi ya kutosha. Tunaheshimu uwezo wa Ndanda, lakini tunataka kushinda."

Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu na itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic