March 31, 2016


Kocha wa Yanga, Juma Mwambusi amesema watacheza kwa umakini mkubwa katika mechi yao ya leo dhidi ya Ndanda.

Mwambusi amesema wanatambua ubora wa Ndanda FC, hivyo umakini litakuwa ni jambo muhimu kwa kuwa hawataki kupoteza mchezo huo wa nusu fainali ya Kombe la Azam Sports HD.

“Kwa sasa hatutaki kupoteza mchezo licha ya ugumu kutokana na ratiba. Lakini tunaanza kupambana na Ndanda ambao ni wazuri sana.

“Tunachofanya ni kucheza kwa juhudi lakini umakini utakuwa ni nguzo,” alisema.


Yanga inaikaribisha Ndanda FC katika mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV