March 31, 2016


Azam FC imetinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho kwa kuichapa Prisons kwa mabao 3-1.

Katika mechi tamu na ya kuvutia kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, timu zilionyesha upinzani mkubwa katika kipindi cha kwanza.

Ulikuwa ni upinzani mkali kati ya timu hizo mbili lakini Azam FC ndiyo waliokuwa makini kuzitumia nafasi walizozipata kupitia Shomari Kapombe aliyefunga mabao mawili na Hamis Mcha aliyefunga moja.

Jeremiah Juma ndiye alifunga bao pekee la Prisons ambayo kila muda ulivyokuwa ukisonga mbele ilionekana kupoteza kasi na umakini.


Azam FC inakuwa ni timu ya tatu kutinga nusu fainali ya Kombe la FA baada ya Mwadui FC na Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV