March 31, 2016




MPIRA UMEKWISHAA
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90, hatari, Minery anapiga shuti kali mpira unagonga mwamba na kutoka nje
SUB Dk 88 Salum Minery anaingia kuchukua nafasi ya Mponda
SUB Dk 84 Nadir Haroub Cannavaro anaingia kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani
KADI Dk 81, Kiggi analambwa kadi ya njano kwa kumwangusha Haji Mwinyi

Dk 80, mpira wa faulo wa Kiggi, unapita sentimeta chache kabisa juu ya lango la Yanga
KADI DK 77, Sibo wa Ndanda analambwa kadi ya njano kwa kushindwa kufunga
Dk 76, Yanga wanafanya shambulizi jingine zuri lakini Ndanda wanaondosha hatari baada ya Ngoma kushindwa kufunga

Dk 74, Ngoma anaingia, moja mbili tatu anapiga shuti lakini kipa Jeremiah Kisubi anadaka vizuri kabisa
SUB Dk 73, Ahmed Msumi anaingia kuchukua nafasi ya Ntebe kwa upande wa Yanga

Dk 72, Sibo analala na kuokoa mpira wa Msuva na kuwa kona
GOOOOOO Dk 69 Yondani anaipiga penalti hiyo vizuri kabisa
na kuandika bao la pili kwa Yanga

PENAAAAT.... KADI Dk 68 Paul Ngalema analambwa analambwa kadi nyekundu kwa kucheza madhambi
KADI Dk 65, Ntebe naye analambwa kadi ya njano kwa utovu wa nidhamu 
Dk 63, Ndanda wanafanya shambulizi jingine, pasi nzuri ya Sibo Aziz lakini krosi ya Atupele inakuwa haina macho

GOOOOOOOO Dk 56 Kiggi Makasi anamchambua Msuva aliyeshuka kusaidia na kufunga bao saaafi kwa shuti kali kabisa
Dk 55, Dida anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti kali
Dk 53, Yondani anaingia vizuri lakini anaanguka mwenyewe, mabeki Ndanda wanaokoa na kuwa kona isiyo na manufaa

Dk 52, Ngoma anaingia vizuri kabisa lakini mpira wake wa krosi unazuiliwa
Dk 49, Atupele naye anajaribu vizuri lakini hata hivyo anashindwa kulenga lango
DK 48, Msuva anapata nafasi nzuri, lakini anapiga shuti kuuuubwaaaaaa
Dk 47, mpira unaonekana kwenda taratibu, hata hivyo bado hakuna mashambulizi zaidi ya pasi nyingi katikati ya uwanja

MAPUMZIKO
DAKIKA 1+ YA NYONGEZA
DK 44, Yanga wanagongeana vizuri na Kaseke anapiga shuti kali, mpira unambabatiza beki mmoja wa Ndanda inakuwa kona isiyo na matunda
Dk 40, mchezo unabadilika na suala la ubabe linatawala
Dk 30 hadi 35, Ndanda wanaonekana kuamka, sasa wanacheza vizuri
GOOOOOO Dk 27 Nonga anafunga bao safi la kichwa akiunganisha mpira wa mpira uliokufa wa Juma Abdul

Dk 23, bado mpira unaonekana umepooza, unachezwa zaidi katikati na mashambulizi ni machache kila upande

Dk 19, Dida analazimika kufanya kazi ya ziada kwa kutoka na kuuwahi mpira miguuni mwa Atupele Green
Dk 13, Kelvin Yondani anapanda juu vizuri na kupiga shuti kali, lakini anapaishaa juuu

DK 8 hadi 11, zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja
Dk 7, Mponda anafunga bao safi pasi ya Lucian, lakini mwamuzi anasema aliotea
Dk 4, Nonga yeye na kipa, anapiga shuti na kumlenga, kipa wa Ndanda naye anapangua
Mpira unaanza, dakika mbili za mwanzo timu zinaonekana kuanza kwa kutegeana.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic