March 31, 2016Mshambuliaji wa Manchester City, Raheem Sterling ameamua kupunguza bei ya jumba lake la kifahari hadj pauni million 1.2.

Awali alitangaza jingo hilo kuwa linapatikana kwa pauni million 3.5, lakini halikupata mteja.

Sterling aliamua kuliuza jumba hilo wakati akiondoka Liverpool na kujiunga na Manchester City.

Jumba hilo la kifahari lina ukumbi wa sinema, bwawa la kuogelea la ndani ambalo lina maji moto, saluni, gym, uwanja wa mpira wa kikapu na uwanja mdogo wa soka.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV