March 30, 2016



Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema ni kazi kubwa sana kwa Yanga kuanzia kesho itakapokuwa inapambana na Ndanda FC katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Akizungumza na SALEHJEMBE jioni hii, Pluijm amesema presha itakuwa kubwa sana kwao kwa kuwa ratiba ya TFF inaibana zaidi timu yake.

"Nimesema kweli kuwa inanishangaza sana. Kesho lazima tucheze na kushinda na kila timu inatupania. Ni hali ngumu sana kwetu.

"Baada ya Kombe la Shirikisho tunarudi kwenye mechi ya ligi ambayo ina presha kubwa tena tukiwa katika maandalizi magumu ya mechi ya kimataifa.

"Sasa hatuna zaidi ya kupambana, sasa tuko kambini na tunajiandaa huku tukiomba tucheze na kumaliza salama," alisema Pluijm.

Yanga inaivaa Ndanda FC katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho linalodhaminiwa na Azam Sports HD kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaaam, kesho.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic