Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja amesisitiza, Simba itaendelea kupambana tena bila ya matatizo pamoja na kwamba beki wake wa kati Abdi Banda, yuko nje.
Banda bado ana kesi ya kumsemea vibaya kocha huyo raia wa Uganda.
“Tuna mechi ngumu zinakuja, zile za Kombe la Shirikisho pamoja na Ligi Kuu Bara. Lakini hatuwezi kuathiriwa na Banda.
“Wanaokuwepo ndiyo wanakuwa kwa ajili ya Simba wakati huo. Kikubwa kwa Simba ni ushirikiano na kucheza kama timu,” alisema Mayanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment