March 30, 2016


Beki wa pembeni wa Simba, Hassani Kessy, amewatoa hofu viongozi wa timu hiyo akiwaambia: “Leteni mkataba wenu.”

Kessy ambaye amekuwa kwenye utata mkubwa katika mkataba wake na timu hiyo, amesema yupo tayari kusaini mkataba na timu hiyo na wale wanaosema amepewa mkataba akakataa kusaini ni waongo.

Beki huyo hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine inayomhitaji kwa ajili ya kusaini mkataba kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Akizungumza, Kessy alisema yeye hana tatizo na Simba na yupo tayari kuongeza mkataba mwingine wa kuichezea timu hiyo kama watafikia makubaliano.

 “Kiukweli kabisa hakuna kiongozi yeyote wa Simba aliyenifuata na kunipa mkataba, zaidi ni tetesi tu zinazozushwa ambazo siyo za kweli.

“Wao hawatakiwi kuongea pembeni, wao wanachotakiwa kukifanya ni kunipa huo mkataba kwa ajili ya kuusoma kwanza huku mazungumzo yakiendelea.


“Sasa ninashangaa kusikia kuwa nimegomea mkataba Simba kitu ambacho siyo sahihi, mimi ni mchezaji halali wa Simba ninayemaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu,” alisema Kessy.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV