Nahodha wa zamani wa Simba, Hassan Isihaka ameamua kunyoa rasta zake.
Isihaka amenyoa rasta ikiwa ni siku chache baada ya kufungiwa kwa mwezi mzima kutokana na kuhusishwa na utovu wa nidhamu baada ya kumjibu maneno yasiyo ya kiungwana kocha wake, Jackson Mayanja.
Leo Isihaka alionekana akiwa ‘siriaz’ na mazoezi kwenye ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam wakati kikosi hicho kikiendelea na mazoezi chini Mayanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment