March 27, 2016



Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema anataka kukutana na kati ya timu tatu katika nusu fainali ya Kombe la FA kwa kuwa anajua ni nyepesi sanaaa.

Julio amezitaja timu ambazo ni laini na nyepesi kuzifunga kuwa ni Yanga, Simba au Azam FC.

Mwadui FC imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kuitwanga Geita Gold Mine inayofundishwa na Selemani Matola kwa mabao 3-0.

“Waje tena Yanga, Simba au Azam FC ndiyo wanafungika kwa ulahisi. Mimi nawajua ndiyo maana nataka tukutane na mmoja wao,” alisema Julio.

Julio ni kati ya makocha wanaojiamini na wameonyesha mfano wa kazi zao kuwa bora licha ya kuhama timu mbalimbali.

Azam, Yanga na Simba bado hazijacheza michezo yao ya robo fainali kwenda nusu fainali.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic