March 16, 2016


Beki wa pembeni wa Azam FC, Shomari Kapombe aonyesha amepania kuweka rekodi katika ufungaji wa mabao baada ya leo kufunga bao la nane.

Kapombe amefunga bao lake la nane katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.

Mabao nane ya Kapombe ni sawa na John Bocco, mshambuliaji na Nahodha wa Azam FC ambaye amewahi kuwa mfungaji bora.

Lakini mabao hayo nane yanamfanya Kapombe kuwa katika nafasi ya nane kati ya wafungaji bora akiwa anazidiwa na watu saba tu. Huku akiwa mfungaji wa pili katika kikosi cha Azam wakati Kipre Tchetche akiongoza kwa mabao 9

Wanaomzidi Kapombe ni kama ifuatavyo:-

Kiiza 18
Tambwe 17
Ngoma 13
Juma J 11
Maguri 10
Tchetche 9
Ajib 9
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV