March 16, 2016
Azam FC imeanza kula viporo vyake vya Ligi Kuu Bara kwa uhakika baada ya kuichapa Stand United kwa bao 1-0 jijini Dar es Salaam, leo.

Ushindi huo umeifanya Azam FC kufikisha pointi 50 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara lakini inaendelea kubaki katika nafasi ya tatu.


Katika mchezo mkali uliochezwa kwenye Uwanja wa Chamazi Complex, Azam FC ilipata bao lake kupitia Shomari Kapombe katika dakika ya 62 baada ya kuunganisha krosi saafi ya John Bocco.

Kabla ya hapo, mechi ilionekana kuwa ngumu humu Azam FC wakipoteza nafasi nyingi za kufunga katika kipindi cha kwanza.


Kipindi cha pili kilianza kwa mashambulizi ya zamu kila upande hadi Azam FC walipopata bao hilo.

Azam FC ilikuwa na michezo mitatu ya kiporo ukilinganidha ya Simba, mchezo mmoja zaidi mkononi ukiwalinganisha na Yanga.

AZAM

Kwa mechi hiyo ya leo, Azam FC imebakiza michezo miwili ya kiporo sawa na Yanga hali ambayo inazidisha presha kubwa kileleni kati ya timu hizo mbili pamoja na vinara wa sasa Simba wenye pointi 54.

STAND0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV