Nigeria imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Misri mjini Kaduna, Nigeria.
Nigeria ndiyo walicheza vizuri zaidi na kupata nafasi nyingi za kufunga kupitia washambuliaji wake, Ahmed Musa, Odion Ighalo, Victor Moses na wengine.
Lakini ikafanikiwa kupata bao katika dakika ya 60 kupitia Oghenekaro Etebo ambaye aliukwamisha mpira wavuni baada ya shuti la Ighalo kugonga mwamba.
Nigeria waliendelea kupoteza nafasi nyingi na wakati inaonekana kama Nigeria wameshinda, Mohamed Salah akasawazisha katika dakika ya 90.
Salah alifunga bao hilo baada ya safu nzima ya ulinzi ya Nigeria kufanya kosa wakidhani ameotea, naye hakuifanyia utani nafasi hiyo.
Kwa sare hiyo, Misri imeendelea kubaki kileleni ikiwa na pointi 7, Nigeria katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 5, Tanzania ya tatu ina pointi 4 na Chad ikiwa mkiani, bila pointi.
0 COMMENTS:
Post a Comment