Mashabiki wa soka, wana mambo yao! Wengi waliojitokeza kuangalia mazoezi ya Taifa Stars kwa siku mbili, wamekuwa wakijadili mambo kadhaa, lakini lile la umbo na ukubwa wa mguu wa mshambuliaji Abdillah Yusuf ‘Adi’ lilichukua nafasi kubwa.
Adi amejiunga na Taifa Stars kwa mara ya kwanza akitokea Mansfield ya daraja la pili nchini England.
Wengi wanaamini Adi anaweza kuwa hatari kwa kuwa anaonekana yuko fiti. Lakini wako wale wanataka kumuona uwanjani kesho akiitumikia Stars ili waone kazi.
Lakini Kocha Abdallah Kibadeni, amesema kwa maana ya mazoezi ya awali anaonekana yuko vizuri lakini hajajua katika purukushani hasa za uwanjani maana hajawahi kumuona akicheza hata mechi ya kirafiki.
0 COMMENTS:
Post a Comment