March 5, 2016


Vijana wawili wa Yanga wanaendelea kuja kwa kasi, Simon Msuva na Salum Telela, wameipa matumaini Yanga kufanya vizuri katika mchezo wao wa leo dhidi ya Azam FC.

Lakini matumaini yameongezeka baada ya mshambulijiaji mkongwe, Amissi Tambwe naye kuanza mazoezini pia.

Juzi Msuva na Telela hawakufanya mazoezi wakiwa majeruhi huku Tambwe akisumbuliwa na mafua lakini jana asubuhi wote walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani.

Pia Ngoma yeye alirejea Yanga mapema wiki hii akitokea kwao Zimbabwe alipokwenda katika msiba wa mdogo wake aliyefariki wikiendi iliyopita baada ya kugongana uwanjani.

Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, alisema wachezaji hao wamerejesha matumaini ya timu yao kufanya vizuri katika mchezo wa leo dhidi ya Azam na ule unaofuata dhidi ya African Sports.

“Nilikuwa kwenye wakati mgumu lakini sasa nimerudi katika matumaini baada ya wachezaji hawa kurejea katika hali zao za kawaida, nina kikosi imara sasa,” alisema Pluijm, raia wa Uholanzi. 


Hata hivyo, Pluijm aliwaomba mashabiki wa Yanga kuendelea kuisapoti timu yao ili iendelee kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara na michuano mingine. Yanga imerejea jana jijini Dar es Salaam kutoka Pemba tayari kwa mchezo na Azam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic