MWADUI FC |
Kikosi cha Mwadui FC kimetinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA linalodhaminiwa na Azam Sports HD kwa kuotwanga GEita Gold Mine kwa mabao 3-0.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mwadui FC waliutawala zaidi mchezo huo kwa vipindi vyote na kuibuka na ushindi huo dhidi ya Geita inayofundishwa na Selemani Matola.
Baada ya mechi hiyo, Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo alisema: “Nilijua tutashinda kwa kuwa tuna kikosi bora kuliko kikosi cha Matola. Nilisikia alisema maneno mengi ya kujisifia, lakini nilijua leo ndiyo mwisho wake katika michuano hii.”
0 COMMENTS:
Post a Comment