March 26, 2016

Kweli ni mwaka wa aibu Coastal Union, sasa imehamia kwa wachezaji wa kigeni baada ya beki na kiungo wake Mcameroon, Sabo Youssoufa kuamua kufunguka kupitia mitandao ya kijamii.

Youssoufa  anaonekana amechoka, anaonekana uvumilivu umemshinda na sasa anataka kurudishiwa pasi yake ya kusafiria pamoja na kulipwa fedha zake za usajili.

SIKU SABO ALIPOSAINI COASTAL KWENYE MEZA YA PLASTIKI...
Viongozi wengi wa Coastal Union wanaonekana kutotaka kupokea simu ili watoe maelezo.

Lakini kiungo huyo kati ya wanaosifika kucheza kwa kujituma, ameomba mashabiki na wanachama wa Coastal Union wajitokeze na kumsaidia.

Timu hiyo kongwe imekuwa ikiongozwa na hadithi za vituko kila kukicha. Hivi karibuni wachezaji waliandamana na kuweka mgomo walipwe mishahara ya miezi mitatu. 


Wakalipwa wa mwezi mmoja tu, lakini wakaonyesha ni wenye nia kwa kuitandika Azam FC. Pia ndiyo timu pekee iliyoifunga Yanga kwenye ligi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic