March 14, 2016


Pamoja na kuichapa Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa mabao 3-0 ikiwa nyumbani kwao Johannesburg, Afrika Kusini, Azam FC imesisitiza, lazima ijiandae vizuri kwa ajili ya mechi ya marudiano jijini Dar.

Azam FC imeitungua Wits kwa mabao 3-0 katika mechi hiyo ya kwanza ya Kombe la Shirikisho. Mechi ya pili itapigwa Jumapili.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi ‘Mbunifu’ amesema wanajua katika soka lolote linaweza kutokea na wanachifanya ni kujiandaa zaidi.

“Mabao matatu ni sehemu ya kujiweka vizuri kwa ajili mechi ijayo. Lazima tucheze mechi ya pili ili tuseme tumefuzu. Hivyo tunajiandaa vizuri sana,” alisema.

Hata hivyo, Mbunifu alisisitiza mechi hiyo imesaidia kuwatangaza wachezaji wa Azam FC kwa kuwa wameifunga timu kutoka katika taifa lililoendelea zaidi kisoka.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV