Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Boniface Ambani amekumbushia namna alivyomzidi ujanja kiungo Mohammed Banka wa Simba na kutoa pasi safi kabisa kwa Benard Mwalala aliyeimaliza Simba.
Mechi hiyo ilichezwa miaka mitano iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Yanga ikaibuka na ushindi wa bao hilo moja.
Ambani raia wa Kenya ambaye alikuwa na kasi sambamba na Mwalala, alimzidi Banka mbio na kutoa krosi ambayo ilionekana kama inatoka, Mwalala akaiwahi kwa “kuslaidi” na kuandika bao saaafi kabisa.
Katika mtandao, Ambani ameeleza ni moja ya siku ambayo inaendelea kubaki kwenye kumbukumbu zake.
0 COMMENTS:
Post a Comment