March 28, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga amesema kikosi chao kina kazi ngumu katika mechi ijayo dhidi ya Al Ahly.

Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi, amesema kikosi cha Al Ahly watakachokutana nacho katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, si timu ndoto.

Lakini anaamini watajiandaa vilivyo, jambo ambalo litazidisha ugumu kwao.

“Sisi pia lazima tujiandae vilivyo, haitakuwa mechi rahisi hata kidogo,” alisema Pluijm leo alipozungumza na SALEHJEMBE.

“Ndiyo maana utaona leo ni sikukuu, tunaendelea na mazoezi. Lazima tuwe na muda wa kutosha ili kuwa vizuri zaidi.”


Yanga imezitoa Circle de Joachim ya Mauritius na APR ya Rwanda na sasa itakutana na Al Ahly ambao ni vigogo waliochukua kombe la ubingwa Afrika, mara nyingi zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV