March 18, 2016

WACHEZAJI STAND UNITED.

Beki wa kati wa Stand United ya Shinyanga, David Assouman N’guessan, raia wa Ivory Coast, hana jezi ndani ya kikosi hicho, kinachofanyika ni kwamba kwenye mechi atakayopangwa basi atavaa jezi ya mchezaji ambaye siku hiyo hachezi kabisa.

Beki huyo mrefu, alijiunga na Stand United katika usajili wa dirisha dogo, Desemba, mwaka jana akitokea Akademi ya OS Abobo iliyopo nchini kwao.

Juzi Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Azam na Stand United uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Muivory Coast huyo alivaa jezi ya beki wa kushoto wa timu hiyo, Abuu Ubwa ambaye siku hiyo hakuwepo kabisa kikosini.

Daktari wa timu hiyo, Abdallah Chuma, amesema kuwa wamekuwa wakifanya hivyo kwenye michezo mbalimbali huku wakiendelea kumtafutia jezi yake kwani zilizopo sasa zote zina majina ya wachezaji wao waliosajiliwa tangu awali.


“Unajua aliposajiliwa hakukuwa na jezi yake na jezi zetu ukiangalia zote zina majina, sasa kuna mpango wa kupata jezi mpya na yeye atapatiwa yake lakini kwa sasa atakuwa akitumia kama ulivyomuona,” alisema Chuma. 

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV