March 16, 2016

ISIHAKA ( WA TATU KULIA) AKISHANGILIA NA WACHEZAJI WENZAKE


Klabu ya Simba, imetangaza kumsimamisha beki wake Isihaka Hassan kwa mwezi mmoja.

Pamoja na kumsimamisha, imetangaza kumvua unahodha msaidizi pale atakaporejea kundini. Hii ni kutokana na madai ya kumjibu kwa lugha isiyo ya kiungwana Kocha wake, Jackson Mayanja alipotaka kumpanda acheze katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Singida United.

Hayo yamesemwa leo na Msemaji wa Simba, Haji Manara wakati alipozungumzia suala la utovu wa nidhamu lililokuwa likimkabiri Isihaka ambaye alisimamishwa kwa muda usiojulikana.

Uamuzi huo wa kumsimamisha ambao ni sehemu ya uamuzi wa kamati ya utendaji, huenda ukasababisha Isihaka kuokosa Ligi Kuu Bara.

Siku Manara alipotangaza kumsimamisha Isihaka kwa muda usiojulikana, mshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza aliandika mtandaoni kwamba mchezaji huyo alikuwa anaonewa na kuchafuliwa jina.

Lakini siku iliyofuata, isihaka alimuabisha Kiiza kwa kuomba radhi kutokana na kosa la kuzungumza kwa lugha isiyo ya kiungwana mbele ya kocha wake na wachezaji wengine.

Uongozi wa Simba ukampa onyo pia na kumtaka azikanushe habari hizo ambazo zilionekana zinalenga kutetea watovu wa nidhamu.2 COMMENTS:

  1. We Saleh Kiiza amekuudhi nini kila kukicha huoni mazuri yake wewe kuandika mabaya tuu,upenzi gani huo?Enyi waandishi na mafarisayo acheni kutumia kalamu zenu vibaya kwani mwisho wake si mzuri!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Una lako jambo wewe,kwani alichokiandika Saleh kibaya kipi kuhusu Kiiza?

      Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV