March 30, 2016


Waamuzi kutoka nchini Ivory Coast wamepewa jukumu la kuchezesha mechi kati ya Yanga dhidi ya Al Ahly jijini Dar es Salaam.

 Pamoja na waamuzi hao kutoka Ivory Coast, kamisaa atakayesimamia mechi hiyo ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika atakuwa anatokea nchini Rwanda.

Taarifa ambazo Championi Jumatano limezipata mwamuzi wa kati atakuwa ni Denis Dimleby atakuwa akisaidiwa na Marios Stan na Mussa Bale watakaoshika vibendera wakati Tango Compo atakuwa mezani.

 Kamisaa ameelezwa kuwa ni Chelistin Ntajaar kutoka nchi ya jirani na Tanzania ya Rwanda.

 Waamuzi hao kutoka Afrika Magharibi, watawasili jijini Dar es Salaam kuanzia Jumatano au Alhamisi siku mbili hadi tatu kabla ya mechi hiyo.


 Mechi hiyo dhidi ya wababe wa Kaskazini mwa Afrika dhidi ya timu kongwe barani Afrika, inasubiriwa kwa hamu kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic