Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limepanga kuwaruhusu mashabiki 40,000 kuingia uwanjani jijini Cairo wakati Misri na Nigeria zikipambana kuwania kucheza Afcon, jana.
Caf kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Misri, imeamua kufanya hivyo na kama mechi hiyo itaisha vizuri, bila ya vurugu zozote, basi uwezekano mkubwa wa mashabiki kupewa ruhusa katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Al Ahly jijini humo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Shirikisho hilo zinaeleza, mashabiki wa soka Misri ndiyo watakaoamua kama mechi ya Yanga ichezwe na mashabiki au la.
Miaka mitatu iliyopita, Yanga iliivaa Al Ahly bila ya kuwa na mashabiki baada ya Caf kuifungia Misri katika suala la mashabiki kuingia uwanjani kutokana na vurugu kubwa zilizosabisha vifo vya mashabiki zaidi ya 10.
Kama mashabiki hao watapata ruhusa, basi Yanga itakuwa na wakati mwingine mgumu kwa kuwa Al Ahly bila ya mashabiki wake kutakuwa na utulivu na mwanya kwa Yanga kufanya vema zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment