March 16, 2016

WITS

Kikosi cha Bidvest Wits kimepanga kutua nchini saa 24 tu kabla ya mechi yao dhidi ya Azam FC katika Kombe la Shirikisho.

Bidvest ambao wanakuja hapa nchini wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kuchapwa mabao 3-0 nyumbani kwao Sauz wiki iliyopita, Jumapili ya wiki hii watashuka dimbani kurudiana na Azam kwenye mchezo wa kombe hilo.

Katibu wa Azam, Idrisa Nassor, amesema taarifa walizozipata ni kuwa wapinzani wao wameamua kutua nchini Jumamosi wakati watacheza Jumapili, hayo yakiwa maamuzi yao binafsi ambapo watakuja na msafara wa watu 30 wakiongozwa na viongozi nane, sambamba na wachezaji 22.

”Sisi tunajua kuwa Bidvest watakuja nchini Jumamosi siku moja kabla ya mchezo wetu wa marudiano baada ya ule wa Sauz ambao tutacheza Jumapili huku tukiwa na idadi ya mabao 3-0 tuliyoyapata kwao.

“Hatujajua sababu ya wao kuamua kutua hapa nchini Jumamosi, kutokana na hayo kuwa maamuzi yao wenyewe waliyoamua ambapo watakuja na jumla ya watu 30,” alisema Nassor.  


Hata hivyo, taarifa nyingine zimekuwa zikisema kuwa wanatarajiwa kutua nchini kesho Alhamisi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV