April 18, 2016

BARCA YAPATA KIPIGO CHA TATU MFULULIZO
Kwa mara nyingine MSN inayoundwa na Suarez, Neymar na Messi imeshindwa kuipa ushindi Barcelona.

Staa Wa Barcelona, Lionel Messi, usiku wa jana aliweka rekodi ya kufikisha mabao 500 tangu aanze kucheza soka lakini rekodi hiyo imekuja na uchungu kutokana na timu yake kupata kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Valencia.

Kipigo hicho ambacho ni cha tatu mfululizo kimekuja wakati mbaya ambapo timu hiyo imekuwa na presha kubwa kwa kuwa imeshatolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia ineonekana kupoteza mwelekeo wa kuwania ubingwa wa La Liga.

Messi akiwa katika masikitiko.
Kipigo hicho cha tatu mfululizo ni cha kwanza kutoka kwa Barcelona tangu ilipotokea hivyo miaka 13 iliyopita, safari hii kikiwa kimetokea kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Camp Nou.

Bao la kujifunga la kiungo wa Barcelona, Ivan Rakitic katika dakika ya 26 lilianza kutibua mipango ya wababe hao wa Hispania kisha kujikuta wakiwa nyuma kwa mabao 2-0 baada ya Santi Mina kutupua wavuni katika dakika ya 45.

Ikumbukwe kuwa timu hizo zilipokutana katika michuano ya Kombe la Copa del Rey, Barcelona ilipata ushindi wa mabao 7-0 kwenye uwanja huohuo, hali ambayo inathibitisha kuwa hali ya mambo siyo nzuri.


Baada ya bao hilo la pili, Barcelona ilionekana ‘kupanic’ na kuanza kutafuta bao kwa nguvu, juhudi hizo zilizaa matunda katika dakika ya 63 kwa Messi kutengeneza nafasi kisha kwenda kuitupia wavuni yeye mwenyewe.

Valencia wakipongezana baada ya kufunga bao.
Mambo yalikuwa magumu kwa Messi.  
Upepo huo mbaya sasa umempa presha zaidi Kocha wa Barcelona, Luis Enrique ambaye timu yake ipo pointi sawa na wabishi Atletico Madrid katika msimamo wa La Liga huku wakiwa pointi moja zaidi ya Rea Madrid.

Katika rekodi ya Messi, bao hilo la jana lilimfanya afikishe mabao 500 tangu aanze kucheza soka la kulipwa ambapo mabao 450 amefunga akiwa Barcelona na 50 katika ngazi ya timu ya taifa ya Argentina ambapo sasa ni nahodha wa timu hiyo.

Kocha wa Barcelona, Luis Enrique akionekana kuchanganyikiwa.
Msimamo wa La Liga kwa timu tatu za juu ulivyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic