Straika wa Arsenal, Welbeck. |
Mshambuliaji
wa zamani wa Newcastle United, Alan Shearer ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa
soka amewaambia Arsenal kuwa hawawezi kutwaa ubingwa wa Premier League mpaka
pale watakaposajili straika wa daraja la kwanza ‘world class striker’.
Nahodha huyo
wa zamani wa England alisema hayo alipokuwa akifanya kazi yake ya uchambuzi
baada ya Arsenal kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Crystal Palace, jana Jumapili.
“Hawawezi
kutwa ubingwa wa ligi mpaka watakapo msajili straika wa kiwango cha juu ambaye
anaweza kufunga mabao 25 au 30 katika msimu mmoja,” alisema Shearer ambaye
alifunga mabao 260 katika Premier League enzi zake alipokuwa akicheza idadi
ambayo hajawahi kufikiwa na mchezaji mwingine yeyote.
“Nimekuwa
nikisema hivyo msimu wote kuwa wanatakiwa kuwa na angalau wachezaji wawili
wenye ubora huo na maoni yangu nana yanaonekana mpaka sasa,” aliongeza.
Kauli hiyo
ni kama mwiba kwa washambuliaji wa timu hiyo akiwemo Mwingereza, Danny Welbeck.
0 COMMENTS:
Post a Comment