April 8, 2016


KIMWAGA (KATIKATI)
Sraika wa Simba, Joseph Kimwaga ametamka kuwa kati ya vitu ambavyo anajutia kwenye maisha yake ya soka, basi ni kutua kuichezea timu hiyo.

Mshambuliaji huyo alitua kuichezea Simba kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Azam FC kwa mkopo, ambapo amekuwa haonekani Simba kwa muda wa mwezi mmoja na nusu kutokana na kutokea sintofahamu kati yake na uongozi.

 Kimwaga alisema alitarajia kufanya mengi makubwa akiwa na Simba, lakini ndoto zake zilikatishwa baada ya kutopewa nafasi ya kucheza.

Amesema Simba ndiyo waliyoifuata Azam kumuomba kwa mkopo na moja ya makubaliano ni kupata nafasi ya kucheza ili akuze zaidi kiwango chake, lakini baada ya kutua mambo yakabadilika.

“Sikutarajia kuyaona haya ninayoyaona hivi sasa Simba, kiukweli siamini, hivyo nimeona ni bora nikae nje ya timu ili nitulize akili yangu kuliko niwe ndani ya timu bila faida.

“Ninajuta kukubali kuja kuichezea Simba, inafikia kipindi ninafikiria vitu vingi sana kwa timu iliyokufuata wenyewe kukuomba kwa mkopo ukakubali halafu baadaye wanafanya vitu sivyo kabisa.

“Nimeona niwaachie timu yao na mimi nifanye mambo yangu mengine huku nikisubiria mkataba wangu miezi mitano na Azam kumalizika, kwa sababu nilifanya kila ninaloliweza ili nipate namba lakini nikashindwa,” alisema Kimwaga.

SOURCE: CHAMPIONI 1 COMMENTS:

  1. Kimwaga hapo Simba bila kutoa 10% ya mshahara wako hupangwi ng'ooo!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV