April 15, 2016


Kiungo na beki wa Simba, Abdi Banda, ametamka kuwa hawaelewi viongozi wa timu hiyo kutokana na ukimya wao juu ya majaaliwa yake kuhusiana na kupewa adhabu au kurejeshwa ndani ya kikosi hicho.

Banda aliondoshwa ndani ya kikosi hicho baada ya kupishana kauli na kocha wake, Jackson Mayanja, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union wiki kadhaa zilizopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, tangu hapo amekuwa nje ya kikosi huku majaaliwa yake yakiwa hayajulikani.


“Nilipeleka barua yangu ya maelezo Machi 28 (mwaka huu), mpaka sasa sijaambiwa chochote. Wamenifungia vioo hawaniambii chochote. Nasikia wameamua kulipeleka suala langu katika Kamati ya Nidhamu ila kwa upande wangu sina hofu yoyote kwa kuwa naendelea kufanya mambo yangu mengine,” alisema Banda.

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Ndio tatizo la viongozi wa simba,kwa kuwa ni mzawa basi hawamjali kabisa.Hivi kuna kosa kubwa kama la kuchelewa kazini bila taarifa yoyote na mbaya zaidi hata mtu ukipigiwa simu hujibu?Imetokea kwa Kiiza na yameisha harakaharaka tu.Na inanilazimisha kuamini pengine sio lugha mbaya tu kwa kocha bali hata ile kadi nyekundu.na kuamini ilisababisha kufungwa na mtani wetu Yanga inachangia.Hebu igeni kwa Yanga,kujali nidhamu kwa wachezaji wote,tukiitwa wa mchangani tunakasirika.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV