April 15, 2016

CHUJI..
Unaweza kuamini hii, kwamba kiungo mkabaji wa Athumani Idd ‘Chuji’ na straika Jerry Tegete, juzi waliwekwa benchi kisa kikiwa ni wao kuwahi kuichezea Yanga?

Wawili hao walikosa mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Yanga ilishinda kwa mabao 2-1.

“Chuji na Tegete makusudi wamewekwa benchi na hawana tatizo lolote, kikubwa ni viongozi walihofia kuwa wangecheza chini ya kiwango kwa kuwa wanakutana na timu yao ya zamani,” kilisema chanzo.

TEGETE
Walipotafutwa wachezaji hao kuzungumzia hilo kwa upande wa Chuji alisema: “Kama unavyojua Anko, mimi nimetokea Yanga kabla ya kuja kuichezea Mwadui, hivyo hiyo sababu inahusika kwa kuwa nipo fiti, kama ningekuwa nina matatizo, basi hata benchi nisingekaa.”


Tegete yeye alisema: “Si unajua tena haya masuala ya soka, kikubwa ninachokiona mimi sikupangwa na kujikuta nikakaa benchi sababu kuwa niliwahi kuichezea Yanga na ndicho kilichoniponza.”

1 COMMENTS:

  1. Julio ana matatizo mbona Jabir Azizi kacheza mechi na simba?Je na huyo golikipa Kado katokea wapi kama si Yanga na hata kadi anayo!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV