April 15, 2016

MAYANJA...
Kocha wa Simba, Jackson Mayanja, ametamka kuwa mkataba wake na Simba unaelekea ukingoni na tayari amepata ofa kutoka kwingine.
 
Mayanja alianza ajira yake hiyo Januari, mwaka huu alipochukuliwa kuwa msaidizi wa Mwingereza, Dylan Kerr lakini hawakufanya kazi kwa kuwa Kerr alitimuliwa kisha Manyanja akapewa jukumu la kusimamia timu.

Tangu ameanza majukumu hayo amefungwa mechi mbili tu dhidi ya Yanga (2-0) na Coastal Union (2-1) kwenye Kombe la FA huku akipata ushindi katika mechi 12.

Mayanja amesema mkataba wake unamalizika mwezi ujao na yupo huru kuzungumza na klabu nyingine yoyote itakayomhitaji kwa sasa.

Amesema pamoja na hivyo, bado anatoa nafasi ya kwanza ya mazungumzo ya mkataba kwa Simba kwa kuwa ndiyo klabu aliyopo mpaka sasa licha ya kuwa amepata ofa kutoka klabu za Afrika Mashariki na Tanzania licha ya kutotaka kuzitaja.

“Sipendi kuweka wazi mkataba wangu ila ni kweli unamalizika mwezi ujao na sijazungumza chochote na Simba kuhusu mkataba mpya mpaka sasa.


“Nitabaki ikiwa uongozi utaamua iwe hivyo lakini kikubwa sitaangalia ushabiki bali kazi, hivyo popote nitakapopata ofa nzuri nitaenda,” alisema Mayanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic