April 15, 2016


SIKU HAJI (KUSHOTO) ALIPOTUA SIMBA...

Beki wa kushoto wa zamani wa Simba, Haji Nuhu ameitwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika Timu ya Ajax inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Nuhu alifungashiwa virago Simba, hivi karibuni ikiwa ni baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa nusu msimu akitokea Azam FC kutokana na kile kilichodaiwa kuwa kiwango chake kilikuwa ni cha chini.

Nuhu amesema nafasi hiyo ameipata baada ya kuunganishwa na wakala wake mwenye uhusiano mzuri na uongozi wa Ajax.

 “Nitaondoka nchini mwisho wa mwezi huu wa Aprili kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio na endapo nitafanikiwa basi nitajiunga na timu hiyo moja kwa moja.


“Namuomba Mungu anijalie afya njema katika kipindi hiki ambacho najiweka fiti ili nitakapofika huko niweze kuwashawishi viongozi hao na wanisajili,” alisema Nuhu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic