April 12, 2016




Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwhelo ametamba kwamba Kombe la FA ni mali yake na ikiwezekana awepe kabla hata ya mechi za nusu fainali.

Mwadui FC imepangiwa Azam FC na itacheza nayo Aprili 24 mjini Shinyanga huku Julio akisema ana imani kubwa, watashinda na kutonga fainali.

"Nilitaka kukutana na Azam au Yanga, najua ni timu nzuri lakini Mwadui FC ina kikosi kizuri na bora zaidi.

"Kama hawataona shida, vizuri wangenipa tu kombe nikae nalo kwanza. Najua nitafika fainali na kulichukua. Watanzania wamesahau, mara ya mwisho wakati Kombe la FA lilipofanyika, nililitwaa mara mbili nikiwa na Tanzania Stars.

"Maana yake lilifia mikononi mwangu, ninaamini litainukia mikononi mwangu na tuko siriaz sana," alisema Julio.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic