April 8, 2016


Kikosi cha Esperance de Tunis ya Tunisia inatarajia kuwasili nchini leo Ijumaa kwa ndege binafsi ya kukodi kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Azam FC huku ikificha idadi ya watu katika msafara wao.

Azam inatarajia kuvaana na Esperance katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, mechi ambayo itachezwa kwenye Uwanja wa Chamazi, keshokutwa Jumapili.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saadi Kawemba, amesema wapinzani wao hao watatua leo usiku na kufikia katika Hoteli ya Bahari Beach.

“Hawajatutaarifu watakuja na kikosi cha watu wangapi kwa kuwa watajihudumia wenyewe,” alisema Kawemba ambaye wiki iliyopita alisema kuwa Esperance wakifika wao Azam watawahudumia kila kitu kwa kuwa wamekubaliana makubaliano maalum ili nao wakienda Tunisia wawahudumie pia.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV