April 7, 2016

MATANDIKA...

Muda mchache baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoa taarifa ya kumsimamisha Juma Matandika, mjadala umeibuka.

Mjadala huo ni kama Matandika alikuwa ni mwajiriwa wa shirikisho hilo, huku wengi wakiamini alikuwa akipiga deiwaka tu.

Wadau wengi wamekuwa wakihoji kuhusiana na Matandika kama kweli ni mwajiriwa au la.

Wengi wa wadau wa soka wamekuwa wakihoji kwa kuwa hawaamini kama TFF ingeweza kumwajiri Matandika.

Lakini ukweli hadi sasa ni mwajiriwa lakini aliyesimamishwa katika cheo chake cha Msaidizi wa Rais Jamal Malinzi.

Hata hivyo, mara zote Malinzi amekuwa akishindwa kufafanya Matandika ni msaidizi wake kwenye nini hasa kwa kuwa shughuli za kiutendaji zinafanywa na katibu mkuu na watendaji wengine kedekede.


Mara kadhaa, SALEHJEMBE imehoji kuhusiana na uweo wa Matandika, nani anamlipa mshahara na uwezo wake faida yake ni nini ndani ya shirikisho hilo, lakini kumekuwa hakuna maelezo ya kutosha.

4 COMMENTS:

 1. Sasa umefurahi Salehe kwa Matandika kutumbuliwa jipu,maana ulienda hadi Handeni Kwachaga kumshughulikia,we noma!

  ReplyDelete
 2. STD SEVEN AND FISH VENDOR AT MAGOMEN MAKUTI, HE ONCE SERVED THE SAM POST WHEN MALINZI WAS SERVING AS YOUNG AFRICANS SECRETARY BEFORE BEING OUSTED.

  ReplyDelete
 3. ALIKUWA AKIKAANGA SAMAKI MAGOMENI MAKUTI PIA MPELEKA MATARUMBETA KUISHANGILIA YANGA AKITOKEA TAWILAYANGA MAKUTI, KATIBU MWENEZI WA CCM KATA YA MAGOMENI

  ReplyDelete
 4. TFF ni taasisi kubwa ambayo katika hali ya kawaida mtu wa aina hii asingeweza kupenya hadi kupewa nafasi ya kumsaidia Rais wa TFF Ofisini.Hivi kweli nchi hii imefikia hatua komandoo wa Yanga au Simba anakuwa Msaidizi wa Rais wa Shirikisho?Mtinginjola aliona mbali lakini hatukumwelewa

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV