April 29, 2016


Straika wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kutokana na kitendo chake cha pamoja na washambuliaji wenzake, kupoteza nafasi nyingi za kufunga katika mechi ya juzi Jumatano dhidi ya Mgambo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara, Yanga ilishinda mabao 2-1 lakini washambuliaji wake walishindwa kutumia nafasi nyingi nzuri walizopata, hali iliyosababisha timu hiyo iwe katika wakati mgumu kwa kuwa Mgambo nao walikuwa wakiwashambulia.

Baadhi ya mashabiki wa Yanga walichukizwa na hali hiyo licha ya timu yao kupata ushindi, ambapo walikuwa wakilalamika wakati mchezo ukiendelea na hata baada ya mchezo huo kumalizika.

Tambwe ameliambia gazeti hili kuwa, hata wao hawakufurahishwa na hali hiyo na ndiyo maana ameomba msamaha.

“Hali hiyo imetuumiza sana hata sisi ndiyo maana kama ulituona baada ya mechi hakuna aliyekuwa na uso wa furaha hata kama tulishinda.

“Ilikuwa simanzi kwetu, nawaomba Wanayanga watusamehe juu ya hali hiyo, tutajipanga na tutakuwa sawa katika mechi zijazo,” alisema Tambwe.


Tambwe alikosa nafasi tatu za kufunga, wenzake Donald Ngoma na Paul Nonga kila mmoja alipoteza nafasi mbili za wazi.

SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV