April 29, 2016Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Simba ilikuwa kisiwani hapa kwa ajili ya kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam FC, lakini baadhi ya mashabiki walionekana wakikishangaa kikosi cha Simba kwa kusema kuwa wachezaji wake wengi wana maumbo madogo.

Mashabiki hao waliokuwa wakifika kwenye Uwanja wa Amaan na Dole kushuhudia mazoezi ya timu hiyo, walikuwa wakibishana kuwa wachezaji hao maumbo yao ni tofauti na yale ya wenzao wa Yanga na Azam ambao asilimia kubwa wana maumbo makubwa.

“Hawa wa Simba wengi wembamba na maumbo yao madogo, lakini wachezaji wa Yanga na Azam wao ni warefu na siyo wembamba kama hawa wa Simba,” alisema shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Ali Omar na kuungwa mkono na wenzake.

Simba ina wachezaji wengi vijana zaidi ukilinganisha na Yanga na Azam FC ambao ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara katika nafasi ya kwanza na ya pili.


1 COMMENTS:

  1. Tatizo lishe,simba lishe duni uwezi kulinganisha na wenzao wakimataifa wanaokula milo kamili!We hukumbuki hata Kaduguda alikuwa anatoa shilingi 6000 kununua maandazi ya wachezaji Simba?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV