April 3, 2016


Wakati Yanga inaisubiri Al Ahly katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Jumamosi.  Tayari harufu ya klabu hiyo kongwe nchini Misri imejaa jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyabiashara wameanza kuuza kama njugu jezi za Al Ahly. Tukio hilo lilitokea leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Wakati Yanga ilikuwa ikipambana na Kagera Sugar katika mechi yake ya Ligi Kuu Bara, pia ikiwa ni maandalizi ya kuivaa Al Ahly, wafanyabiashara hao walikuwa jukwaani wakiuza jezi hizo.

Hata hivyo, wafanyabiashara hao wasingeweza kuuza jezi hizo katika jukwaa la Yanga maana ingekuwa mtiti, nao walilijua hilo kwa kuwa walikuwa wakiendelea kuziuza katika jukwaa lenye mashabiki wa Simba.

1 COMMENTS:

  1. Sasa mashabiki wa Simba wakivaa jezi za Al ahly ndio itazuia Yanga kutoa kichapo?Walichapwa APR mbele ya wanajeshi wao waliovalia sare za jeshi itakuwa wao?AL AHLY WATACHAPWA TU.MUNGU IBARIKI YANGA.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV