April 13, 2016


Kikosi cha Yanga kinachotarajia kushuka uwanjani leo kupambana na Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, tayari kimeanza kuchukuwa tahadhari kuelekea mechi yake ya kimataifa dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Timu hiyo itaondoka nchini hivi karibuni kwenda Misri kupambana na Al Ahly katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika baada ya ule wa kwanza uliofanyika wikiendi iliyopita jijini Dar kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Katika mazoezi ya Yanga yaliyofanyika jana asubuhi kwenye Uwanja wa Gymkhana, kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm alitumia saa moja na nusu kukinoa kikosi hicho kwa kuwapatia mbinu mbalimbali wachezaji wake na zaidi ilikuwa katika upigaji wa penalti.

Ikumbuke kuwa mwaka 2014, Yanga ilipokutana na Al Ahly katika mechi yake ya pili ya michuano hiyo huko nchini Misri ilitupwa nje kwa mikwanju ya penalti 4-3.

Hali hiyo ndiyo inayoonekana kumfanya Pluijm aanze kuchukua tahadhari mapema ya kukabiliana na changamoto zote atakazokutana nazo katika mechi hiyo ya marudiano inayotarajiwa kupigwa Aprili 19, mwaka huu.


Katika mazoezi hayo ya kupiga penalti wachezaji wote wa kikosi hicho waliokuwa mazoezini hapo walifanya vizuri isipokuwa, Pato Ngonyani, ambaye alishindwa kukwamisha mpira wavuni mara mbili.


Kuhusu mikwaju hiyo ya penalti, Pluijm alisema kuwa: “Siyo kwamba tunajiandaa kwa ajili Al Ahly bali huo ni utaratibu wetu wa kila siku tunapokuwa mazoezini.”

2 COMMENTS:

  1. Wanajiandaa kwa mechi zingine kwani ya Al Ahly imeshakwisha hapa nyumbani.Kule ni kwenda kutimiza wajibu wasije wakafungiwa na CAF tuu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapana,na tuikatae hiyo dhana maana kwenye mpira lolote laweza tokea,Kama ni mfuatiaji wa habari za michezo kwa vyombo vya nje utaona kabisa katika mchezo wa yanga na waarabu yanga ndio wamepewa sifa ya kucheza vizuri zaidi kiasi kwamba wengi wanaamini Yanga wanaweza kuwatoa waarabu kama tu watakuwa makini na hatua ya matuta.Binafsi sio shabiki wa yanga lakini naamini kama watakuwa makini watafanya vizuri maana hata hao waarabu wana mchecheto na Yanga

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic