April 13, 2016

KAGERA SUGAR

Sasa mambo safi kwa Kagera Sugar, maana wanaweza kurejea nyumbani kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na hiyo ni baada ya vifaa vya kukamilisha uwanja huo kuwasili nchini.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kagera, Salum Umande Chama, amesema kuwa moja ya vifaa hivyo vya kukamilishia uwanja ni magoli ambayo ndani ya siku kumi na nne yatakuwa yameshawekwa.

“Nadhani hautakuwa na siku nyingi kutoka sasa. Vifaa vya mwisho nimepata taarifa leo hii (juzi Jumamosi) kuwa vimefika bandarini na kwa mujibu wa injinia (mhandisi) itamchukua siku 14 kumaliza kila kitu.


“Kilichokuwa kinakwamisha ni hivyo vifaa lakini kwa kuwa vimewasili, naamini siku chache kutoka sasa utakuwa tayari kwa matumizi,” alisema mwenyekiti huyo wa Kamati ya Waamuzi kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

2 COMMENTS:

  1. Vifaa vilishawasili zaid ya miez 4 ilopita,tatizo ni mafundi,baada ya vifaa kuchelewa bandarini waliondoka kwenda S.Africa,vifaa vilipoletwa bkb kutoka bandarini jamaa hawajatokea.
    Na muda wa kukamulisha ni siku 14 tu ila ndo hivyo.
    Mussa bkb

    ReplyDelete
  2. Vifaa vilishawasili zaid ya miez 4 ilopita,tatizo ni mafundi,baada ya vifaa kuchelewa bandarini waliondoka kwenda S.Africa,vifaa vilipoletwa bkb kutoka bandarini jamaa hawajatokea.
    Na muda wa kukamulisha ni siku 14 tu ila ndo hivyo.
    Mussa bkb

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV