April 7, 2016


Mshambuliaji nyota wa zamani wa Arsenal, Nwankwo Kanu leo ametembelea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam na kusema anaumizwa na wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo.


Kanu aliwahi kulazimika kupumzika kucheza soka kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Akiwa Muhimbili alitembelea pia wodi ya wagonjwa wa moyo na kupata maelezo kutoka kwa madaktari bingwa.

Kanu yuko nchini katika ziara iliyoandaliwa na kampuni ya StarTimes Tanzania ambayo yeye ni balozi.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV