April 7, 2016

RAIS TFF, JAMAL MALINZI

Zaidi ya wadau 168 waliotuma maoni yao kwenye email ya blog hii, wamempata Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuachia ngazi.

Mashabiki hao 168 ni kati ya 231 waliotuma maoni yao na kusema litakuwa ni jambo la msingi akiachia ngazi kutokana na sakata la masuala ya rushwa linaloiandama TFF kwa sasa.

Maofisa wawili wa TFF, wanashutumiwa kupanga matokeo baada ya sauti yao kunaswa wakipanga mipango ya rushwa tena waziwazi.

Pia tayari maofisa wawili wa TFF wamekwenda baada ya mmoja kujiuzulu na mwingine kusimamishwa kazi.

Aliyejiuzulu ni Martin Chacha aliyekuwa mkurugenzi wa mashindano na Msaidizi wa Rais, Juma Matandika naye amesimamishwa.

Mashabiki hao wanaona Malinzi hana sababu ya kubaki TFF kwa kuwa uongozi wake tayari umepoteza mwelekeo.

Wengi wamedai wanaotuhumiwa ni watu waliokuwa chini yake, aliyekuwa anafanya nao kazi akiwemo msaidizi wake, hivyo vema naye akakaa kando.


Wengine wasiozidi 33 wamesisitiza kuwa Malinzi anaweza hawana jibu sahihi abaki au aondoke na 30 waliobaki, wamesisitiza hawatamani hata kumuona na hawataki kumzungumzia kwa kuwa TFF ya sasa imefeli.

2 COMMENTS:

  1. Sasa unadhani kampeni zako za kumng'oa Malinzi ili mfadhiri wako Ngumbaro apate nafuu kwa kufungiwa kwake itafanikiwa?Ama kweli nimeamini wewe ni mganga njaa na mpiga dili mkubwa kwa kutumia kalamu yako!Endelea

    ReplyDelete
  2. Tusilete mzaha kwenye jambo la aibu kwenye soka letu kwa kumtetea Malinzi.Hoja iliyopo mezani ni sakata la rushwa katika soka la Tanzania yeyote aliyehusika anapaswa kuwajibishwa, ni suala la kuondoa wote waliohusika kuchafua taswira ya mchezo wa soka hapa nchini.FIFA wameweza kumuondoa Bltter inakuwaje Tanzania ishindwe?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV