April 10, 2016


MURO
Kauli aliyoitoa Msemaji wa Yanga, Jerry Muro wakati akihojiwa na EFM Radio imezua mjadala mkubwa kwenye mitandao.

Muro alitoa kauli hiyo wakati aliposema kuwa ana uhakika Simba hawawezi kuwa mabingwa wa Kombe la Shirikisho wala Tanzania Bara.

Alisema wao Yanga walipanga kuwasaidia, lakini kwa kuwa wamewashangilia Al Ahly katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana, kamwe hawatakuwa mabingwa.

Kauli hiyo imekuwa mjadala kwenye makundi mengi ya Whatsapp na Facebook, wengi wakihoji kama Yanga na Simba kusaidiana katika kubeba ubingwa.

Lakini wengine wanahoji, kwamba kauli yake inaonyesha kwamba walijiandaa kupanga matokeo kwa kuwa timu moja kuisaidia nyingine kuwa bingwa, ni kupanga matokeo.


Hata hivyo, mvutano ni mkali, hakuna anayekubali upande mmoja na wengine wanaona sawa huku wengine wakipinga kuhusiana na hilo.

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV