April 12, 2016



Wakati wa lile tamasha la kila mwaka la Majimaji Selebuka, ni rasmi sasa mwaka huu litafanyika kati ya Mei 28 mpaka Juni 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini Songea, Ruvuma.

Tamasha hilo linaloratibiwa na Taasisi ya Songea & Mississippi (Somi) hujumuisha michezo pamoja na shughuli mbalimbali za kijamii, likiwa na lengo la kuibua vipaji vya michezo na kuwainua Watanzania mkoani humo.


Mratibu wa tamasha hilo, Reinafrida Rwezaura alitaja shughuli matukio yatakayokuwepo kuwa ni pamoja na mashindano ya mbio za baiskeli, ngoma za asili, raidha, utalii wa ndani, maonyesha ya ujasiriamali na biashara pamoja na midahalo ‘debate’ kwa shule za sekondari.

Aliongeza, tofauti na mwaka jana, mwaka huu kutakuwa na washriki kutoka nchi za nje kama vile Malawi, Msumbiji na Zambia.


“Maandalizi yapo tayari cha msingi ni watu kutuunga mkono kwa kujitokeza kushiriki kwenye tamasha hilo maana ni faida ya kila mtu. Kupitia tamasha hili, Tanzania inaweza kupata wanamichezo wazuri sana.

"Kupitia maonesha ya ujasiriamali watu watapata nafasi ya kutangaza  biashara zao, bahati nzuri kuna baadhi ya makampuni makubwa hapa nchini yamekubali kutupa sapoti, kwa hiyo mjasiriamali atakuwa na fursa ya kutangaza biashara yake,” alisema Reinafrida 

Pamoja na kuwa limefanyika mara moja tu, tamasha hilo limejizolea umaarufu mkubwa hasa Kusini mwa Tanzania.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic