April 12, 2016


Baada ya siku 1065 za kusubiri ukarabati wa uwanja wao, wakiwa ‘wanadoea’ viwanja vingine mashabiki wa Besiktas wamerejea kwenye Uwanja wao wa Vodefone Arena.

Uwanja mpya, safi pembezoni mwa jiji la Istanbul, tena uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 43,000. Jukwaa lake moja, situ zake hazipatikani uwanja wowote duniani.


Katika kila siti katika jukwaa hilo, shabiki anakuwa anaona pia kupitia TV iliyo mbele yake, yaani nyuma ya siti ya mbele yake kama inavyokuwa kwenye ndege au mabasi ya kisasa.

Ana nafasi ya kuangalia mechi au marudio ya slow motion kwa karibu zaidi. Hiyo ndiyo kazi ya Waturuki.

Nchini humo, timu kubwa zaidi ni Galatasaray, inafuatiwa na wapinzani wao wakubwa Fenerbahce halafu Besiktas.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV