April 25, 2016

KIONGERA
Straika aliyetarajiwa kwa makubwa, Mkenya, Paul Rapahel Kiongera, punde tu baada ya Ligi Kuu Bara kumalizika, atakuwa huru na breki ya kwanza ni kurudi kwao Kenya kupumzika mwezi mzima kabla ya kuanza mchakato kwingine.

Hata hivyo, amefunguka mazito baada ya kuweka wazi kuwa anajuta kuja Bongo hasa timu kubwa (ikiwemo Simba) kwani alionywa na rafiki yake wa karibu na kiungo wa zamani wa Azam, Humphrey Mieno.

Kiongera amesema hata kwa hirizi, hawezi kubaki Tanzania hata kama atatakiwa na timu gani huku akisema Bongo imerudisha nyuma ndoto zake za maisha.

“Si Simba wala timu yoyote, lakini hata hivyo mimi kubakia Tanzania ama kuwaza siku moja nirudi kucheza hapa ni ndoto! Kaka ni vigumu nisikufiche.

“Niliambiwa na Hump (Humphrey) kuhusiana na soka la Tanzania hasa kwa timu kubwa lakini ndiyo hivyo na mbaya zaidi nilikuwa nimeshasaini mkataba, ila nimejifunza mengi,” alifunguka kwa simanzi.

Kiongera alionekana tishio mwanzoni ambapo mchezo wake wa kwanza Msimbazi akitokea KCB ya Kenya, aliingia kambani mara mbili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Gor Mahia, mchezo wa maandalizi ya msimu 2014/15, lakini aliumia katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Coastal na kulazimika kufanyiwa upasuaji nchini India kabla ya kupelekwa kwa mkopo KCB ambapo aliendeleza moto wa kutupia mabao.

Hata hivyo, anaamini hajaisha, bali hapewi nafasi ya kuonyesha kiwango chake.


“Hivi unawezaje kunihukumu wakati sichezi? Sijapewa nafasi tangu nimerejea. Nimeanza katika mechi moja tu, sijapewa nafasi tu lakini Kiongera ni yuleyule na nitafanya makubwa tu,” aliongeza.

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Hapo Simba kuna jipu kubwa linatakiwa kutumbuliwa!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic