April 25, 2016



Mashabiki wa Yanga wamepewa somo kuwa wanatakiwa kubadilika kama wanataka timu hiyo iweze kufanya vizuri katika mechi zake za Ligi Kuu Bara zilizobakia, lakini pia zile za kimataifa ambazo kikosi cha timu hiyo kitacheza hivi karibuni.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kutua nchini wakitokea Misri walipokuwa wameenda kupambana na Al Ahly katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wakizungumza kuhusiana na nguvu za mashabiki, washambuliaji wa timu hiyo, Amissi Tambwe na Simon Msuva, walisema mashabiki wa Yanga wanatakiwa kubadilika na kuachana na tabia ya kuwazomea wachezaji pindi wanapokuwa uwanjani wakiitumikia klabu hiyo.

Walisema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwafanya washindwe kujiamini, ndiyo maana wamekuwa wakishindwa kufanya vizuri wanapocheza nyumbani kutokana na kuwa na hofu ya kuzomewa lakini pia kutukanwa.

“Siyo sisi tu ambao hali hiyo inatuumiza lakini ni wachezaji wengi, ndiyo maana ukiangalia mechi zetu nyingi za kimataifa, tulizocheza nyumbani hatukufanya vizuri ila tulizocheza ugenini tumecheza kwa kiwango kikubwa.


“Unajua nini, ni kwa sababu kule hakuna mashabiki, kwa hiyo tunakuwa na uhuru wa kucheza bila ya presha ya mashabiki na kama mtu akikosea hakuna wa kumvunja moyo, hivyo anaongeza bidii ya kupambana,” alisema Tambwe akiungwa mkono na Msuva.

 Nyota hao katika mechi zilizopita za kimataifa zilizofanyika hapa nchini, walikuwa wakikumbana na changamoto nyingi kutoka kwa mashabiki wa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic