April 16, 2016



Beki wa Mwadui FC, Iddy Mobby alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumatano.

Mobby alionyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu kwa mara ya pili straika wa Yanga, Donald Ngoma ndipo mwamuzi Selemani Kinugani kutoka Morogoro akamtoa nje.

Sasa kali zaidi ni kwamba, Kocha wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumfutia beki wake huyo kadi hiyo nyekundu akidai alionyeshwa kimakosa.

Julio alisema kuwa Kinugani alimwonyesha Mobby kadi hiyo kimakosa kwa sababu yeye siyo aliyemchezea faulo Ngoma kwani aliyefanya hivyo ni kiungo wake Razack Khalfan.

“Kadi nyekundu aliyopewa Mobby ilikuwa ni ya uonevu kwani si yeye aliyemchezea faulo Ngoma bali aliyekuwa amefanya hiyo ni Razack, hivyo naiomba TFF imfutie adhabu hiyo mchezaji wangu,” alisema Julio.

Razack naye alipoulizwa alisema: “Kweli mwamuzi alimuonea Mobby kwani mimi ndiye niliyemchezea faulo Ngoma kwani alikuwa anakwenda kutufunga.”


Hata hivyo, picha za video za mchezo huo zinaonyesha wazi kuwa Mobby ndiye aliyemchezea rafu Ngoma hivyo kuzima madai hayo ya Julio na Razack.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic